Saturday, November 29, 2014

MARUBANI 3 WA JESHI LA POLISI WAFARIKI PAPOHAPO BAADA YA KUPATA AJALI YA HELIKOPTA JIJINI DAR.Tazama hapa..

at 1:23:00 PM  |  No comments

Sehemu ya mabaki ya Helikopta baada ya kuanguka 

Ajali ya Helicopter ya Maliasili na Utalii imegharimu maisha ya marubani 3 wa Jeshi la Polisi Tanzania. 

Sp Kidai Kaluse, Insp.Simba Must Simba, Pc. Josso Selestine, Na rubani mmoja Capt. Khalfan,Ajali  hiyo imetokea huko Kipunguni B Moshi Bar,Ukonga-Ilala jijini Dar es Salaam. Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikaa mpaka sasa.

 Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova
akifafanua jambo mbele ya Vyombo vya habari katika eneo la ajali,kufuatia kutokea kwa ajali hiyo iliyopelekea vifo vya watu wanne
 Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaa,Mh.Sadick Meck Sadick akizungumza mbele ya Vyombo vya habari katika eneo la ajali,kufuatia kutokea kwa ajali hiyo iliyopelekea vifo vya watu wanne
 Baadhi ya Wataalamu wakifanya uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo ya Helikopta.
 Baadhi ya Watu wakishuhudia mabaki ya helikopta hiyo iliyopata ajali maeneo ya Kipunguni B Moshi Bar,Ilala jijini Dar es Salaam.

Share
Posted by Unknown
About the Author

Write admin description here..

0 comments:

Text Widget

Blogger templates. Proudly Powered by Blogger.