Na Dotto Mwaibale
KIWANDA cha A Two Z kilichopo Arusha kimeingia katika kashifa ya kumnyima ruhusa mfanyakazi wake aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria ambaye alifia kiwandani hapo kwa kukosa huduma.
Mfanyakazi aliyefia katika kiwanda hicho kilichopo eneo la Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha ametajwa kuwa ni Mohamed Abbas.
Tukio hilo linadaiwa kutokea Aprili 18 mwaka huu baada ya mfanyakazi huyo kunyimwa ruhusa na viongozi wake hivyo kupoteza maisha yake baada ya kuzidiwa na maumivu ya kichwa.
Akizungumza na Jambo Leo kwa njia ya simu na sharti la kutotaja jina lake mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho alidai kuwa kitendo alichofanyiwa mwenzano ni cha kinyama hivyo akaomba jambo hilo lisifumbiwe macho hata kidogo kwani linaweza kutokea na kwa mwingine.
"Baada ya kukataliwa kupewa ruhusa Aprili 20 mwaka huu aliendelea na kazi huku akilalamika kuumwa lakini baadae hakuonekana kiwanda hadi mwili wake ulipokutwa ukitoa harufu kali zaidi ya wiki moja.
Kijana huyo alikutwa akiwa amefariki katika Idara ya VHI Garment kitengo cha Balling ambapo mazishi yake yalifanyika katika makaburi ya Daraja Mbili.
Meneja Uzalishaji wa Kiwanda hicho,Hassan Atako alipo ulizwa juu ya madai hayo alisema hawezi kuzungumza chochote kuhusu suala hilo kwa kuwa si msemaji.
Jitihada za gazeti hili za kumpata Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha ili kuzungumzia suala hilo hazikuzaa matunda baada ya simu yake ya mkononi kuita kwa muda mrefu bila ya kupokelewa baada ya kupigiwa.
Chanzo Arusha yetu
0 comments: