Viongozi wa ngazi za juu wa Tanzania leo wameelekea katika maeneo
mbalimbali hasa ya jiji la Dar es Salaam kuona kwa karibu uharibifu
uliofanywa na mvua kali zilizonyesha kwa siku kadhaa mfululizo na
kusababisha mafuriko makubwa.
Huku Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifanya ziara yake mkoani Morogoro kukagua maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko, Makamu wa Rais Dk Gharib Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, wamefanya ziara ya kutembelea maneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam.
Watu wasiopungua 13 wameripotiwa kupoteza maisha na mamia ya wengine kupoteza makazi yao kufuatia mvua hizo kali zilizoanza siku ya Ijumaa. Habari nyingine zinasema kuwa, Makamu wa Rais Dk Gharib Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova wamenusurika katika ajali ya helikopta baada ya helikopta hiyo ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) waliyokusudia kuitumia kukagua maeneo ya mafuriko kupata ajali Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Viongozi hao wameamua kufanya ziara yao hiyo kwa kutumia gari baada ya ajali hiyo.
Maelezo zaidi yamo kwenye ripoti hii hapa chini ya mwandishi wa Radio Tehran jijini Dar es Salaam.

0 comments: