Wednesday, July 27, 2016

Ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali yawataka wananchi kuheshimu tunu za Taifa

at 1:36:00 PM  |  No comments

http://nicemediaworkstz.blogspot.com/
Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw. Kassian Chibogoyo (kulia) akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) rangi sahihi zinazotakiwa kutumika katika bendera ya Taifa wakati akielezea umuhimu wa wananchi kutumia vielelezo sahihi vya Taifa na kuachana na vile vya kughushi, kulia ni Afisa Habari toka Idara ya Habari (Maelezo) Bw. Frank Shija.

Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw. Kassian Chibogoyo (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa wananchi kutumia vielelezo sahihi vya Taifa na kuachana na vile vya kughushi, kushoto ni Afisa Habari toka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Nyamagori Omarihttp://nicemediaworkstz.blogspot.com/
Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw. Kassian Chibogoyo (katikati) akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) baadhi ya vielelezo sahihi vya Taifa vinavyotakiwa kutumiwa na wananchi wakati alipokuwa akielezea umuhimu wa wananchi kutumia vielelezo sahihi vya Taifa na kuachana na vile vya kughushi mapema hii leo Jijini Dare s Salaam kulia ni Afisa Habari toka Idara ya Habari (Maelezo) Bw. Frank Shija na kushoto ni Afisa Habari toka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Nyamagori Omari.Picha zote na Eliphace Marwa - Maelezo


Na: Frank Shija, MAELEZO

Katika kuhakikisha heshima , hadhi na maadili miongoni mwa jamii ya Watanzania Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi mahiri wa Rais John Pombe Magufuli imewakumbusha wananchi kuheshimu na kuzingatia matumizi sahihi ya Vielelezo vya Taifa.

Haya yamebainishwa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Cassian Chibogoyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Kipindi chake cha ‘Tujikumbushe’’ Sehemu ya Pili kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Chibogoyo amesema amesema kuwa wakati sasa umefika kwa jamii kuendeleza utamaduni uliokuwapo wa kuheshimu na kufuata desturi zilizowekwa katika kuendeleza umoja, amani na mshikamano. ‘Natoa wito kwa watanzania wote, katika kufanya maboresho ya kurejesha hadhi ya taifa tunapaswa kuheshimu sana Vielelezo vya Taifa letu, hapa na maanisha tuheshimu wimbo wa taifa na Nembo ya Taifa.’

Amesema kuwa katika kuhakikisha vielelezo hivyo vinaheshimiwa Ofisi yake imejipanga kufuatilia kwa karibu wale wote watakao kiuka matumizi sahihi ya Vielelezo vya Taifa ikiwemo Nembo, Bendera na Wimbo wa Taifa.

Aliongeza kuwa kuanzia sasa matumizi ya Bendera ya Taifa yatakwenda sambamba na matumizi ya Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki hivyo amezitaka Ofisi zote za Serikali pamoja na Taasisi zake waanze utaratibu wa kupandisha pia bendera hiyo kwani Tanzania tunaamini katika ushirikiano huo.

Katika hatua nyingine uongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu (TUGHE) Tawi la Ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali wamekanusha tuhuma zilizoandikwa na moja ya gazeti hapa nchini(Jina limehifadhiwa) zikimtuhumu Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kuwa na kusema kuwa tuhuma zilizoandikwa katika Gazeti hilo siyo zakweli na ata wao kama wafanyakazi wameshangazwa

Katibu wa TUGHE Tawi la Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali amesema kuwa ni vyema waandishi wakafanya kazi zao kwa weledi kuliko kuandika taarifa zizizosahihi kwani kufanya hivyo kuta waingiza matatizoni. Nilitegemea kabla mwandishi hajachapisha habari ile angetafuta ukweli kutoka upande wa pili ikiwemo kuhusishwa kwa uongozi wa Chama cha Wafanyakazi kwani ndiyo wenye mamlaka yakutoa taarifa katika ngazi husika kwa tupo kwa ajili ya kuwawakilisha na kuwatetea wafanyakazi.

Kipindi cha Tujikumbushe kimekuwa kikionyeshwa na TBC1 ambapo lengo lake kuu ni kutoa elimu kwa jamiii juu ya matumizi sahihi na umuhimu wa kutunza nyaraka na tunu za Taifa, ambapo Sehemu ya Kwanza ya kipindi hicho kilihusu Nyaraka za Serikali. Kipindi kinachofuata kitahusu Historia ya kuwepo kwa Katiba na Katiba inayopendekezwa

Share
, Posted by Unknown
About the Author

Write admin description here..

0 comments:

Text Widget

Blogger templates. Proudly Powered by Blogger.