Thursday, June 23, 2016

Mhariri mkuu wa gazeti la Dira asimamishwa kazi

at 2:59:00 PM  |  No comments

Mkurugenzi Mkuu wa gazeti la Dira Alex Msama, amemsimamisha kazi aliyekuwa Mhariri wa Habari wa Gazeti  hilo la Dira ya Mtanzania Mussa Mukama kutokana na mapungufu ya kiutendaji kwa kuonesha dhahiri kutomudu nafasi hiyo.
Msama pia amemuomba radhi Waziri wa Sheria na katiba, Dk. Harrison Mwakyembe kufuatia habari mbili zilizochapishwa kwenye lake, mbele ya waandishi wa habari Msama amekubali kuwa habari hiyo iliyobeba kichwa cha habari Utapeli wa Mwakyembe wamwagwa hadharani haikufuata misingi ya uandishi wa habari.
Hivi karibuni Waziri Mwakyembe aliitisha mkutano wa waandishi wa habari mjini Dodoma akilalamikia kuwa habari mbili za gazeti hilo zilizochapishwa na Gazeti la Dira  ya Mtanzania la June 20 na la June 23 mwaka huu zililenga kumchafua na kuahidi kulishtaki gazeti hilo kupitia habari hizo mbili

Share
, Posted by Unknown
About the Author

Write admin description here..

0 comments:

Text Widget

Blogger templates. Proudly Powered by Blogger.