Mjumbe
wa baraza la jiji la Dar es Salam, Halima Mdee akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na mali zilizopo jiji la Dar es
Salaam kuwa zipo chini ya jiji la Dar es Salaam. Kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita.
Mjumbe
wa baraza la jiji la Dar es Salam, Saed Kubenea akionyesha baadhi ya
nyaraka za siri za jiji la Dar es Salaam ambazo wameanza kuzichambua
kwaajili za kutambua mali zilizo chini ya jiji la Dar es Salaam.
katikati ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita na Afisa habari wa Ukawa, Gasto Makwembe.
Kushoto ni Mstahiki
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kuanza kuchunguza mali za
jiji la Dar es Salaam, (Katikati) Mjumbe wa baraza la jiji la Dar es
Salam, Halima Mdee na Kulia ni Mjumbe wa baraza la jiji la Dar es Salam, Saed Kubenea wakiwa katika mkutano wa Meya wa jiji la Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
BARAZA
la Madiwani la Jiji la Dar es Salaam limeunda kamati ya kuchunguza mali
za jiji hilo kutokana na mali hizo kugubikwa na mbinu chafu na jiji
kushindwa kunufaika mali hizo.
Akizungumza
leo na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Mstahiki Meya wa Jiji la
Dar es Salaam, Isaya Mwita amesema kuwa kamati hiyo lazima ichambue
mali hizo na kama ziko kwenye mikataba nazo ziangaliwe jinsi
walivyoingia.
Amesema
kuwa katika mali hizo ni pamoja na vibanda 130 vilivyo katika Benjamin
Mkapa Kariakoo waliopanga vibanda hivyo wanalipa sh.30,000 ambapo kwa
kiwango hicho ni kidogo sana kutokana eneo vilipo.
Mwita
amesema kuwa mali za jiji zimekuwa hazinufaishi na kufanya mapato
kukusanywa sh.bilioni 11.7 hivyo mali zote zikichambuliwa jiji
linaweza kukusanya zaidi ya sh.bilioni 20.
Aidha
amesema kuwa UDA ni mali ya jiji kutokana na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG) kuzungumza kuwa shirika la Uda ni mali ya
jiji.
Mwita
amesema vyanzo vingine ambavyo jiji haipati fedha ni Soko la Kariakoo,
DDC hivyo vikiamgaliwa na kamati iliyoundwa itaonyesha hali halisi na
jinsi jiji watavyonufaika.
0 comments: