Kamishna
Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya
(kushoto) akiwa na waliokuwa Wafanyakazi wa Benki ya StanBic Tanzania,
Sioi Sumari (katikati) na Shose Sinare, wakiwa Mahakam ya Hakimu Mkazi
Kisutu, Jijini Dar es salaam.
Washitakiwa
hao wanaokabiriwa na mastaka nane likiwemo la utakatishaji Fedha kiasi
cha Dola za Marekani milioni 6, ili kufanikisha mkopo kutoka Benki ya
Stanbic kwenda Serikalini, walifikishwa Mahakamani hapo leo kusikiliza
keshi yao, na walifanikiwa kufutiwa Shitaka moja la kutakatisha Fedha
kati ya nane yaliyokuwa yakiwakabili, ambapo Washitakiwa hao walisomewa
kufutwa kwa shitaka hilo kwa madai ya kukosa Vidhibitisho.
Aidha
mpaka mtandao huu unatoka Mahakamani hapo Mawakili walikuwa bado
wakihangaikia kupata dhamana kufutiwa shitaka hilo lililokuwa na kikwazo
kikubwa cha dhamana
Baada ya kufutiwa shitaka hilo, DPP aliwasilisha hati ya mapendekezo ya kukata rufaa ya kupinga uamuzi wa kufuta shitaka namba nane la utakatishaji Fedha linalowakabili watuhumiwa hao, ambapo zoezi la dhamana liligonga mwamba na Washitakiwa hao wamerudishwa rumande.

0 comments: