Na Anitha Jonas – MAELEZO
Waziri
Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania Mheshimiwa Kassim
Majaliwa amewahakikishia wawekezaji kutoka Vietnam kuwepo kwa fursa za
uwekezaji nchini.
Majaliwa
ameyasema hayo jana katika kongamano la ujumbe wa Rais wa Vietnam
Mheshimiwa Troung Tan Sang pamoja na wadau wa uwekezaji kutoka nchini
humo ambapo wanatarajia kufanya ziara ya siku nne nchini wakitazamia
fursa za uwekezaji nchini.
“Nchi
yetu inamazingira mazuri ya uwekezaji, usalama wakutosha na pia kuna
uhahika wa soko kwani ipo mikataba ya kikanda ya kukuza masoko katika
nchi wanachama kama EAC na SADC kwani katika nchi hizo kuna watu zaidi
ya milioni 300”, alisema Majaliwa.
Akiendelea
kuzungumza na wawekezaji hao Waziri Mkuu alisema serikali ya Tanzania
imekuwa ikiboresha Mazingira ya uwekezaji nchini na hiyo imechangia
ongezeko la wawekezaji.
Mbali
na hayo Majaliwa alisema serikali imekuwa ikiboresha sheria na
kuimarisha ushirikishwaji wa wadau wa sekta binafsi lengo likiwa ni
kuchochea mazingiraya uwekezaji ikiwa ni kuimarisha uchumi wa taifa
pamoja na kukuza kipato cha kila mtanzania.
Hata
hivyo Waziri Mkuu aliipongeza Kampuni ya VIETTEL Tanzania Ltd kutoka
Vietnam ambayo imewekeza katika Sekta ya Mawasiliano kwani imewasaidia
watanzania wengi wa vijijini kupata mawasiliano.
0 comments: