Bw. Javier Rielo
ametoa ahadi hiyo leo tarehe 14 Machi, 2016 alipokutana na kufanya mazungumzo
na Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar es salaam.
Mradi huo
utahusisha ujenzi wa bomba lenye urefu wa kilometa 1,410 ambalo litasafirisha
mafuta ghafi kutoka ziwa Albert nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga na utarajiwa
kuzalisha ajira za moja kwa moja 1,500 na ajira zisizo za moja kwa moja 20,000.
Katika Mazungumzo
hayo Bw. Javier amemueleza Rais Magufuli kuwa Kampuni yake inatarajia kutumia
dola za kimarekani karibu bilioni 4 ambazo tayari zimeshaandaliwa.Pamoja na
kuukaribisha uwekezaji huo mkubwa kwa Tanzania, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameitaka
kampuni hiyo kuharakisha mchakato wa kuanza kwa mradi, na ameshauri muda wa
miaka mitatu uliopangwa kuukamilisha mradi huo upunguzwe, ili manufaa yake
yaanze kupatikana mapema.
Kwa upande wake
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, amesema Wizara yake ipo
tayari kuhakikisha mradi huo unafanikiwa, na itatoa ushirikiano wa kutosha
kuharakisha utekelezaji wake.
Prof. Mhongo
amebainisha kuwa licha ya kwamba hali ya kijiografia, hali ya hewa na bandari
ya Tanga vinatoa mazingira bora ya kufanikiwa kwa mradi huo, Tanzania pia
inatarajia kunufaika na bomba hilo, kwa kuwa kuna tafiti mbili za mafuta zinazoendelea
katika ziwa Tanganyika na katikati mwa Tanzania, ambazo zikikamilika kwa
mafanikio inatarajiwa bomba hilo litasaidia kusafirisha mafuta yake.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es
salaam
0 comments: