Friday, August 15, 2014

Inasikitisha sana..MWANAFUNZI ALIWA NA MBWA HADI KUFARIKI DUNIA,WANANCHI WAMKAMATA MBWA HUYO NA KUMCHOMA MOTO..Chungulia Hapa

at 3:21:00 AM  |  No comments





MWANAFUNZI wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Ludewa iliyopo katika mkoa wa Njombe, Ibrahim Faraja (9), amekufa kwa kuliwa baadhi ya nyama za mwili wake na Mbwa wawili wanaosadikika kuwa na ugonjwa wa kichaa cha Mbwa kwa kukosa chakula kwa muda mrefu.

Taarifa zinasema tukio hilo limetokea Agosti 8, saa saba mchana katika eneo la Ikulu, ambapo marehemu akiwa pamoja na wenzake wawili wasiotambuliwa majina mara moja walikuwa wakipita njia karibu na nyumba ya, Bosco Lingalangala, kwenda kuchuma matunda aina ya mapera ndipo walipoanza kukimbizwa na Mbwa hao ambapo wenzake wawili walifanikiwa kukimbia na yeye kuanza kuburuzwa na Mbwa kichakani.


Padri


Taarifa kutoka ndani ya Hospitali ya wilaya ya Ludewa, zinasema uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa mwili wa marehemu ulikuwa na majeraha makubwa katika sehemu za paja la mguu wake wa kulia likiwa limeliwa na kuondolewa nyama pamoja na nyama za kwenye makalio.




Moto

Wananchi wakichoma moto Mbwa hao baada ya kuuwawa kwa kupigwa risasi na Jeshi la Polisi


“Tumeitisha mkutano na wananchi wamesema hawataki kuishi pamoja na huyo mmiliki wa hao Mbwa kutokana na mwendendo wake anavyoenenda licha ya kuwa ni mzawa wa eneo hili ila hitimisho litapatikana kwenye kikao kijacho ambacho hatujajua kuwa tutakifanya lini”.

Kamanda wa polisi mkoani Njombe, Fulgensi Ngonyani, amesema usalama wa wananchi hao uko salama na kuwa Jeshi hilo limejipanga kukabiliana na vitisho hivyo kwani  Jeshi hilo limeanza utaratibu wa kumhoji mmiliki wa Mbwa hao.





Upande mwingine hofu imetanda Urambo tokana na mbwa wenye kichaa  KUNDI la Mbwa wenye Kichaa limezuka katika Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, na kuifanya wilaya hiyo kufanya msako wa kuua Mbwa wanaozagaa mtaani ili kudhibiti ugonjwa huo kufuatia mtu mmoja kung’atwa na kufa kwa ugonjwa huo na kusababisha hali ya taharuki kwa baadhi ya wakazi wake. Afisa Mifugo wa Halmashauri hiyo, Dkt. Liobu Boya, amesema Mbwa hao wanawapa ugumu wa kuwawinda kwa kuwa baadhi ya watu huwafungia ndani pindi wanaposikia msako uko mitaani mara kwa mara. Amesema hadi sasa wamewauwa mbwa wapatao ishirini (20), na kuwa wameamua kufanya msako wa kuwaua mbwa hao kwa siku nne mfululizo, ambapo kwa siku ya jana na leo wamesema hawajafanikiwa kuona mbwa wengine wanaozagaa mtaani. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Adam Malukwi, amesema ni lazima zoezi la kuwaua mbwa hao liendelee ili kuwadhibiti mbwa wote wanaozurura sanjari ambao wanasababisha madhara kwa binadamu na mifugo kuwangata na kufa kwa kuambukizwa ugonjwa wa kichaa cha mbwa. Akizungumza na blog hii  mmoja wa watu waliojeruhiwa kwa kung’atwa na Mbwa hao, Yona Elisante, amesema kuwa Mbwa hao wamekuwa wakiwang’ata watu wazima na watoto hivyo kupelekea kutibiwa kwa gharama kubwa na wakati mwingine hushindwa kupata fedha za matibabu. Hata hivyo, baadhi ya wakazi mkoani Tabora wameitaka serikali kuharakisha zoezi la utoaji chanjo kwa mbwa hao ili kupunguza tatizo hilo na kama ikishindikana wananchi wapewe ruhusa ya kuwaua kwa njia mbalimbali zinatazo wezesha kuondoa tatizo hilo. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwanzugi katika Wilaya ya Igunga, Samweli Hashimu, amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema kuwa mpaka sasa watu watatu katika kijiji hicho wamejeruhiwa kwa kung’atwa na mbwa hao huku akisema wanaendelea kuwa kutishio kwenye mtaa huo na viunga vyake. Katika kipindi cha hivi karibuni baadhi ya matukio ya watu kung’atwa na Mbwa katika maeneo mbalimbali nchini yaliripotiwa katika kipindi hicho ambapo tafiti zilionyesha kuwa ugonjwa huo unaongoza kwa kuua watu wengi duniani licha ya jitihada zinazofanywa na Serikali kwa kutoa chanjo ya kuchanja mbwa hao bure katika maeneo mbalimbali nchini.chanzo FIKRA PEVU

Share
Posted by Unknown
About the Author

Write admin description here..

0 comments:

Text Widget

Blogger templates. Proudly Powered by Blogger.