NiceMediaWorks
Home
Posts
Email
MATUKIO
HABARI
MAGAZETI
MAKALA
BURUDANI
AFYA
PRODUCTION
INJILI
Style Icons
MAWASILIANO
Top 10 List
Friday, April 25, 2014
HII NI MPYA ASKARI WA JESHI LA POLISI AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUTUHUMIWA KUIBA MTOTO
at 12:18:00 AM | 
No comments
Askari anaetuhumiwa kuiba mtoto akizibwa na polisi wenzie waandishi wasimpige picha
ASKARI wa Jeshi la Polisi na raia mmoja wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Wilaya ya Mbeya wakituhumiwa kwa makosa mawili ambayo ni kula njama za kutenda kosa pamoja na wizi wa mtoto.
Watuhumiwa hao ni pamoja na Mshtakiwa wa kwanza aliyekuwa Ditektivu Constebo wa Polisi mwenye namba WP 5367 Prisca Isaya (35) mwenyeji wa Ilala Dar es salaam ambaye hata hivyo alivuliwa vyeo na kufukuzwa kazi kabla ya kupandishwa Mahakamani na Salehe Mwangosi (28) mkazi wa Njisi wilayani Kyela Mkoa wa Mbeya.
Akisoma mashtaka yanayowakabiliMwendesha mashtaka wa Serikali, Juliana William, mbele ya Hakimu wa Wilaya yaMbeya, Maria Batulaine, alisema watuhumiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa namakosa mawili waliyoyatenda Aprili 4, Mwaka huu.
Alisema kosa la kwanza ni kula njama kwa nia ya kutenda kosa la kuiba mtoto kinyume cha kifungu cha 384 (16) cha kanuni ya adhabu kilichofanyiwa marejeo mwaka 2002 walilofanya Aprili 4, Mwaka huu katika eneo la Songwe wilayani Kyela.
Alitaja kosa la pili kuwa ni Wizi wa mtoto kinyume cha kifungu cha 169 (1) (a) sura ya 16 ya kanuni ya adhabu kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Mwendesha mashtaka huyo aliiambiaMahakama kuwa washtakiwa wote kwa pamoja mnamo Aprili 6, Mwaka huu katika eneola Zahanati ya Njisi Wilaya ya Kyela Mkoani hapa kwa maksudi waliiba mtotomwenye umri wa siku saba kutoka kwa mama yake mzazi Mboka Mwakikagile.
Washtakiwa wote kwa pamoja walikana kuhusika na tukio hilo ambapo upande wa mashtaka ulidai upelelezi wa shauri hilo umekamilika na upo tayari kuwaleta mashahidi wake kwa ajili ya kuendelea na usilizwaji wa kesi.
Kwa upande wake Hakimu aliahirisha kesi hadi Mei 6, Mwaka huu na kwamba dhamana kwa washtakiwa iko wazi kama watakidhi vigezo ambavyo ni kila mmoja kuwa na wadhamini wawili wenye mali zisizo hamishika zenye thamani ya shilingi Milioni 5, barua ya mtendaji na barua kutoka kwa mwajiri kwa ajili ya mshtakiwa wa kwanza.
Hata hivyo walishindwa kuwa na wadhaminiwaliokidhi vigezo vya mahakama na kuamliwa kurudishwa rumande hadi Mei 6, Mwakahuu kesi itakapo kuja kwa ajili ya kusikilizwa.
Share
MATUKIO
Posted by Unknown
About the Author
Write admin description here..
«Newer Post
Older Post»
0 comments:
About Me
Unknown
View my complete profile
NiceMedia. Powered by
Blogger
.
BOFYA HAPA LIVE NICEMEDIA RADIO
Radio ya Injili inayoburudisha na Kuelimisha
Popular
Recent
Comments
Tags
Popular Posts
KWENYE MECHI YA SIMBA NA YANGA KUNA VITUKO...Hivi ndivyo ilivyokuwa Bofya hapa ujioneeeee
HII NI AJALI MBAYA SANA ILIYOHUSISHA MABASI 2 KUGONGANA USO KWA USO NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU 30 PAPOHAPO..Samahani kwa picha
Mkutano wa Ulaya na Afrika waanza Brussels
MWIGULU NCHEMBA AANZA SAFARI YA KUHAKIKISHA WAFUGAJI WANAACHA KUFUGA KIHOLELA,WAFUGE KWA VITALU.
Tazama HIVI NDIVYO MAADHIMISHO YA MIAKA 51 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YALIVYOFANA....Bofya hapa.....
Labels
Afya
BURUDANI
Favourite
Gear
HABARI
HABARI ZA INJILI
HIVI PUNDE
MAGAZETI
MAKALA
MATUKIO
nice studio
SIASA
slider
TANGAZO
Nice Media work Tz
Latest tweets
Latest Videos From NiceMedia Prod.
Search
BLOG RAFIKI
Udaku Special
MillardAyo
Jiachie
Text Widget
© 2013
NiceMediaWorks
.
Woo Themes
converted by
Bloggertheme9
Blogger templates
. Proudly Powered by
Blogger
.
0 comments: