waandamanaji Ukrain |
Kwa mujibu wa ripoti, waandamanaji wametaka nao kuitishwa kura ya maoni kwa ajili ya kujitenga na kujiunga na shirikisho la Russia kama lilivyofanya hivi karibuni jimbo la Crimea sanjari na kurejeshwa madarakani Viktor Yanukovych kama Rais wa halali aliyechaguliwa na wananchi wa nchi hiyo.
Kwa upande mwingine, maelfu ya wananchi wamejitokeza mjini Kiev, mji mkuu wa Ukraine wakiunga mkono viongozi wa sasa na kutaka kudumishwa umoja wa kitaifa nchini humo. Hayo yanajiri katika hali ambayo suala la kujitenga eneo la Crimea kutoka Ukraine na kujiunga na Russia limeendelea kushadidisha uadui kati ya Moscow na nchi za Magharibi.
0 comments: