NiceMediaWorks
Home
Posts
Email
MATUKIO
HABARI
MAGAZETI
MAKALA
BURUDANI
AFYA
PRODUCTION
INJILI
Style Icons
MAWASILIANO
Top 10 List
Saturday, March 29, 2014
kuzisha hati Milioni moja wakimbia machafuko Sudan Kusiniwa
at 12:27:00 PM | 
No comments
Umoja wa Mataifa umetoa tahadhari mpya kuhusiana na kuzidi kuwa mbaya hali ya kibinadamu huko Sudan Kusini huku mapigano yakizidi kushtadi kati ya vikosi vya serikali na vile vya waasi watiifu kwa Makamu wa zamani wa Rais wa nchi hiyo Riek Machar.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imeeleza katika ripoti yake kuwa zaidi ya watu milioni moja wamebaki bila makazi tangu vita na machafuko yalipozuka nchini humo mwezi Disemba mwaka jana.
“Katika muda wa siku 100 tangu ulipoanza mgogoro nchini Sudan Sudan, zaidi ya watu milioni moja wameyakimbia makaazi yao”, imeongeza ripoti hiyo ya OCHA.
Ripoti hiyo aidha imefafanua kwamba licha ya usitishaji vita uliotangazwa mwezi Januari, mapigano makali yangali yanaendelea kati ya vikosi vya serikali na vile vya upinzani katika maeneo kadhaa yakiwemo majimbo ya Jonglei, Unity na Upper Nile.
Umoja wa Mataifa umeonya pia kupitia ofisi yake ya uratibu wa masuala ya kibinadamu kuhusu kuzidi kuwa mbaya hali ya usalama wa chakula katika maeneo ya mgogoro. Kwa mujibu wa ripoti ya OCHA watu wasiopungua milioni
tatu
na laki saba wanakabiliwa na hatari ya kukosa chakula.
Maelfu ya watu wameuawa na wengine wengi kubaki bila makaazi kutokana na mapigano ya zaidi ya miezi mitatu kati ya vikosi vya serikali ya Sudan Kusini na vile vya waasi watiifu kwa Makamu wa zamani wa Rais wa nchi hiyo Riek Machar…/
Share
HABARI
Posted by Unknown
About the Author
Write admin description here..
«Newer Post
Older Post»
0 comments:
About Me
Unknown
View my complete profile
NiceMedia. Powered by
Blogger
.
BOFYA HAPA LIVE NICEMEDIA RADIO
Radio ya Injili inayoburudisha na Kuelimisha
Popular
Recent
Comments
Tags
Popular Posts
Maajabu haya TAZAMA MAITI ZA WATU ZILIZO KAUSHWA NA KUTUPWA..Tazama picha hizi
MASANJA MKANDAMIZAJI MSANII MWENYE MAFANIKIO MAKUBWA..SOMA HAPA.
TAZAMA JINSI AJALI ZA PIKIPIKI ZINAVYOLETA BALAA
Tamasha la Pasaka ni jambo kubwa kwetu.Asema DC Geita
Waziri Nape ni faraja Tamasha la Pasaka Mwaka huu
Labels
Afya
BURUDANI
Favourite
Gear
HABARI
HABARI ZA INJILI
HIVI PUNDE
MAGAZETI
MAKALA
MATUKIO
nice studio
SIASA
slider
TANGAZO
Nice Media work Tz
Latest tweets
Latest Videos From NiceMedia Prod.
Search
BLOG RAFIKI
Udaku Special
MillardAyo
Jiachie
Text Widget
© 2013
NiceMediaWorks
.
Woo Themes
converted by
Bloggertheme9
Blogger templates
. Proudly Powered by
Blogger
.
0 comments: