Wednesday, March 26, 2014
Watu 11 wafariki katika milipuko ya mabomu Nigeria
at 2:19:00 AM |  No comments
Watu wasiopungua 11 wakiwemo maafisa watano wa polisi wameuawa katika miripuko miwili ya mabomu iliyotokea katika eneo lililoathiriwa na machafuko huko kaskazini mashariki mwa Nigeria. Miripuko hiyo ya mabomu ilitokea huko Maiduguri makao makuu na mji mkubwa zaidi katika jimbo la Borno kwa kupishana dakika kadhaa. Msemaji wa polisi Gideon Jibrin ameeleza kuwa raia watatu waliuawa baada ya gari moja kuripuka na maafisa watano wa polisi walifariki dunia baada ya bomu la pili lililokuwa limetegwa kwenye gari la polisi kuripuka dakika kumi baada ya mripuko wa kwanza. Msemaji huyo wa polisi ameongeza kuwa hata hivyo bado hawajafahamu iwapo watu wengine watatu waliouliwa kwenye mripuko wa pili walikuwa ni wategaji mabomu hayo au la. Mbali na miripuko hiyo ya jana, watu wengine 20 waliuliwa pia Jumapili wiki hii katika mripuko uliotokea kwenye soko moja huko Bama katika jimbo la Borno.
Share
Posted by Unknown
-
UNESCO KUENDELEZA UTAMADUNI WA KUZISAIDIA REDIO JAMII
-
Watu 11 wafariki katika milipuko ya mabomu Nigeria
-
Kenya's Nairobi commuters face chaos amid taxi fees protest
-
MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO TAZAMA HII
-
Makubwa haya??RAIS WA KOREA APIGA MARUFUKU MTU YEYOTE KUTUMIA JINA LAKE ASEMA WOTE WENYE MAJINA YANAYOFANANA NA LAKWAKE WAKAYAFUTE KWA KUAPA MAHAKAMANI..Tazama hiii

0 comments: