NiceMediaWorks
Home
Posts
Email
MATUKIO
HABARI
MAGAZETI
MAKALA
BURUDANI
AFYA
PRODUCTION
INJILI
Style Icons
MAWASILIANO
Top 10 List
Tuesday, March 25, 2014
Mgogoro wa Syria utaenea nchi zote za eneo.
at 1:46:00 PM | 
No comments
Amir wa Kuwait Jaber Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah, amezionya nchi za eneo la Mashariki ya Kati kutokana na vita vya nchini Syria. Amir wa Kuwait ambaye nchi yake mwenyeji wa kikao cha hivi sasa cha viongozi wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, ameyasema hayo katika hotuba aliyoitoa leo katika kikao hicho na kuongeza kuwa, kila kundi ambalo linadhania kuwa halitaguswa na athari mbaya za mgogoro wa Syria, lijue kuwa linakosea, kwani mgogoro huo utaenea katika nchi zote za eneo hili. Al-Jaber Al-Sabah ameongeza kuwa, kuna haja ya kurejeshwa mgogoro wa Syria katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kulitaka baraza hilo kumaliza maafa ya nchi hiyo. Amir wa Kuwait ameongeza kuwa, hivi sasa eneo la Mashariki ya Kati lingali linakabiliwa na jinai za kigaidi na kwamba, kuna haja ya kufanywa juhudi thabiti za kupambana na ugaidi. Hayo yanatolewa katika hali ambayo katika kikao hicho, Salman bin Abdulaziz Aal Saud, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudia, ametaka kuungwa mkono zaidi makundi ya kigaidi nchini Syria na kusisitiza kuwa, kiti cha Syria katika kikao hicho kinatakiwa kukabidhiwa kwa mkuu wa muungano wa wapinzani nchini Syria. Kikao cha wakuu wa nchi za Kiarabu kimeanza leo nchini Kuwait chini ya anga ya mfarakano mkubwa kati ya baadhi ya nchi za Kiarabu. Kikao hicho kitajadili hali ya mambo nchini Syria, Libya, Yemen, Palestina na kadhalika suala la kupambana na ugaidi.
Share
Posted by Unknown
About the Author
Write admin description here..
«Newer Post
Older Post»
0 comments:
About Me
Unknown
View my complete profile
NiceMedia. Powered by
Blogger
.
BOFYA HAPA LIVE NICEMEDIA RADIO
Radio ya Injili inayoburudisha na Kuelimisha
Popular
Recent
Comments
Tags
Popular Posts
South Africa links Rwanda diplomats to attacks
Kenya anti-terrorism squad gets $735 a month
Waislamu waendelea kuuawa na Anti-Balaka CAR
kuzisha hati Milioni moja wakimbia machafuko Sudan Kusiniwa
PITIA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI DECEMBER 15, 2016
Labels
Afya
BURUDANI
Favourite
Gear
HABARI
HABARI ZA INJILI
HIVI PUNDE
MAGAZETI
MAKALA
MATUKIO
nice studio
SIASA
slider
TANGAZO
Nice Media work Tz
Latest tweets
Latest Videos From NiceMedia Prod.
Search
BLOG RAFIKI
Udaku Special
MillardAyo
Jiachie
Text Widget
© 2013
NiceMediaWorks
.
Woo Themes
converted by
Bloggertheme9
Blogger templates
. Proudly Powered by
Blogger
.
0 comments: