NiceMediaWorks
Home
Posts
Email
MATUKIO
HABARI
MAGAZETI
MAKALA
BURUDANI
AFYA
PRODUCTION
INJILI
Style Icons
MAWASILIANO
Top 10 List
Wednesday, March 26, 2014
Wakimbizi wa Kisomali watakiwa kurejea kambini
at 2:22:00 AM | 
No comments
Kenya Jumanne hii imewaamuru wakimbizi wa
Somalia
wanaoishi mijini kurudi katika kambi zao katika juhudi za kukomesha mashambulizi ya wanamgambo wa ash Shabab yanayotekelezwa kulipiza kisasi dhidi ya hatua ya Kenya ya kutuma wanajeshi wake katika nchi jirani ya Somalia.
Joseph Ole Lenku, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya ametoa agizo hilo akiashiria changamoto za dharura za kiusalama katika miji ya Kenya, hata hivyo hatua hiyo huwenda ikakabiliwa na ukosoaji wa makundi ya kutetea haki za binadamu ambayo huko nyuma yalipinga hatua kama hizo.
Waziri wa Mambo
ya
Ndani wa Kenya amesema kuwa wakimbizi wote wa Kisomali wanaoishi nje ya kambi maalumu za Kakuma na Daadab kuanzia sasa wanatakiwa kurudi kwenye kambi zao hizo na kwamba yeyote atakayekiuka agizo hilo atafunguliwa mashtaka.
Lenku pia amesema kuwa vituo vyote vya kuwasajili wakimbizi huko Nairobi, Mombasa, Isiolo huko kaskazini na Nakuru kaskazini magharibi vitafungwa. Amewataka pia Wakenya wote kuwaripoti wakimbizi au wahamiaji wowote haramu watakaopatikana nje ya kambi hizo.
Share
Posted by Unknown
About the Author
Write admin description here..
«Newer Post
Older Post»
0 comments:
About Me
Unknown
View my complete profile
NiceMedia. Powered by
Blogger
.
BOFYA HAPA LIVE NICEMEDIA RADIO
Radio ya Injili inayoburudisha na Kuelimisha
Popular
Recent
Comments
Tags
Popular Posts
South Africa links Rwanda diplomats to attacks
Kenya anti-terrorism squad gets $735 a month
Waislamu waendelea kuuawa na Anti-Balaka CAR
kuzisha hati Milioni moja wakimbia machafuko Sudan Kusiniwa
PITIA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI DECEMBER 15, 2016
Labels
Afya
BURUDANI
Favourite
Gear
HABARI
HABARI ZA INJILI
HIVI PUNDE
MAGAZETI
MAKALA
MATUKIO
nice studio
SIASA
slider
TANGAZO
Nice Media work Tz
Latest tweets
Latest Videos From NiceMedia Prod.
Search
BLOG RAFIKI
Udaku Special
MillardAyo
Jiachie
Text Widget
© 2013
NiceMediaWorks
.
Woo Themes
converted by
Bloggertheme9
Blogger templates
. Proudly Powered by
Blogger
.
0 comments: