NiceMediaWorks
Home
Posts
Email
MATUKIO
HABARI
MAGAZETI
MAKALA
BURUDANI
AFYA
PRODUCTION
INJILI
Style Icons
MAWASILIANO
Top 10 List
Friday, June 27, 2014
NHC yaendesha jukwaa la Uwekezaji katika Sekta ya Nyumba kwa wadau wake.Bofya hapa..
at 2:15:00 AM | 
No comments
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mh.Prof Anna Tibaijuka akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wadau mbalimbali kwenye jukwaa la Uwekezaji katika Sekta ya Nyumba.Prof.Tibaijuka alisema kuwa Serikali inaridhishwa na utendaji unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Alisema katika kipindi kifupi Shirika limefanya mageuzi makubwa kwenye sekta ya makazi na kwamba miradi hiyo itakapokamilika,itaifanya miji hiyo kuwa ya kisasa.Prof.Tibaijuka alisema kuwa kampuni za uwekezaji kwenye sekta ya nyumba ni muhimu na hunyanyua uchumi wa nchi,alisema kuwa ili Taifa liweze kuendelea ni lazima liwe na mipango miji na kwamba kupanga miji sio kukata viwanja bali ni kunahitaji mambo mengi.Prof Tibaijuka amewataka wananchi kuwa tayari katika suala la kupanga miji,na maeneo yote yatakayopangwa ni lazima yafidiwe.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC,Nehemia Mchechu akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wadau mbalimbali kwenye jukwaa la Uwekezaji wa sekta ya nyumba lililofanyika jijini Dar.Bwa.Mchechu alisema kuwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),limedhamiria kuyabadilisha maeneo ya jiji la Dar na mikoa mingine nchini baada ya kuzindua ujenzi wa miji midogo.
Alisema kuwa Miradi hiyo itakapokamilika itabadilisha mandhari ya maeneo mbalimbali nchini na kuyafanya kuwa ya kisasa,Mchechu alisema kuwa wataanza na miradi mitatu ikiwemo miji midogo katika majiji ya Dar es salaam na Arusha na kuendeleza nyumba zao zilizobomolewa.
Alisema kuwa katika jiji la Dar,watakuwa na mradi wa salama Kigamboni na Kawe mbayo italifanya jiji hilo kubadilika kuwa la kisasa,aliongea kuwa katika miradi hiyo,kutajengwa nyumba nyingi za kuishi, biashara na sehemu za huduma muhimu .
Mchechu amesema kuwa mradi mwingine utakaotekelezwa ni wa Usa River Safari City utakaojengwa jijini Arusha,ambao utalenga kulibadilisha jiji hilo na kuwa la kisasa,aliongeza kusema kuwa mradi huo utagharimu dola za Kimarekani bilioni mbili (zaidi ya shilingi bilioni 3.4) na itakamilika kati ya kipindi cha miaka saba mpaka 12.Bwa.alisema kuwa miradi mingine ambayo itatekelezwa ni pamoja na Bagamoyo,Dodoma,Mbeya,Mtwara,Lindi,Mwanza na maeneo Mengine.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),Bi.Zakhia Meghi akizungumza kwa ufupi mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wadau mbalimbali kwenye jukwaa la Uwekezaji wa sekta ya nyumba.
Sehemu ya meza kuu ikifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye jukwaa hilo la uwekezaji wa sekta ya Nyumba,lililofanyika jijini Dar
Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye kwenye jukwaa la Uwekezaji wa sekta ya nyumba.
Share
MATUKIO
Posted by Unknown
About the Author
Write admin description here..
«Newer Post
Older Post»
0 comments:
About Me
Unknown
View my complete profile
NiceMedia. Powered by
Blogger
.
BOFYA HAPA LIVE NICEMEDIA RADIO
Radio ya Injili inayoburudisha na Kuelimisha
Popular
Recent
Comments
Tags
Popular Posts
South Africa links Rwanda diplomats to attacks
Kenya anti-terrorism squad gets $735 a month
Waislamu waendelea kuuawa na Anti-Balaka CAR
kuzisha hati Milioni moja wakimbia machafuko Sudan Kusiniwa
PITIA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI DECEMBER 15, 2016
Labels
Afya
BURUDANI
Favourite
Gear
HABARI
HABARI ZA INJILI
HIVI PUNDE
MAGAZETI
MAKALA
MATUKIO
nice studio
SIASA
slider
TANGAZO
Nice Media work Tz
Latest tweets
Latest Videos From NiceMedia Prod.
Search
BLOG RAFIKI
Udaku Special
MillardAyo
Jiachie
Text Widget
© 2013
NiceMediaWorks
.
Woo Themes
converted by
Bloggertheme9
Blogger templates
. Proudly Powered by
Blogger
.
0 comments: