NiceMediaWorks
Home
Posts
Email
MATUKIO
HABARI
MAGAZETI
MAKALA
BURUDANI
AFYA
PRODUCTION
INJILI
Style Icons
MAWASILIANO
Top 10 List
Monday, June 9, 2014
HATARI: Miaka 50 ya Uhuru..Walimu 97 watumia choo kimoja; wanafunzi 3,563 watumia matundu 14
at 5:31:00 AM | 
No comments
WALIMU 97 katika shule ya msingi Nyankumbu na Mkombozi katika Wilaya ya Geita, wanatumia tundu moja la choo ambacho kipo kwenye nyumba ya mwalimu huku wanafunzi wa shule hizo 3,563 wakitumia matundu 14 ya choo na kuhofiwa kutokea magonjwa ya milipuko.Taarifa za awali kuhusu tatizo hilo zinadai kuwa, baadhi ya walimu wamekuwa wakiulalamikia uongozi wa halmashauri hiyo kwa muda wa miaka mitano hadi sasa, bila kusikilizwa licha ya uongozi wa shule kuandika barua kwa Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kutaka tatizo hilo kutatuliwa.
Baadhi ya wanafunzi wakiongea na mtandao huu Juni 6, 2014 wamedai kuwa wamekuwa wakipata usumbufu wakati wa kujisomea kutokana na shule hizo kukosa madawati yakutosha na wakati mwingine kuhofia kula vyakula mbalimbali kutokana na hofu ya kupata magonjwa ya milipuko.
Akizungumzia tatizo hilo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi, Nyankumbu, Jasmin Ngume, amesema awali ilikuwa shule moja na baada ya muda uongozi wa Halmashauri hiyo, ilifanya utaratibu wa kuzigawanya na kuwepo na shule ya msingi Mkombozi na Nyankumbu, ambazo hadi sasa zinakabiliwa na matatizo ya miundombinu ya madarasa na vyoo.
“Tangu walivyofanya utaratibu wao tumeendelea kutumia tundu moja kwa walimu wote lakini wanafunzi waligawana matundu Saba kwa kila shule” alisema Ngume.
Shule zetu
Amesema kwa mujibu wa taratibu za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, uwiano wa vyoo kanuni zinaeleza kuwa walimu wa kiume wanne wanatakiwa kutumia tundu moja na walimu wa kike watatu wanatakiwa kutumia tundu moja, na wanafunzi wakiume watatu hutumia tundu moja na wakike wanne hutumia tundu moja jambo ambalo halipo katika shule hiyo.
“Hili tatizo limekuwa kubwa kwa maana wakati mwingine wanafunzi wamekuwa wakienda kujisaidia kwenye nyumba za majirani na wakati mwingine wanazuiliwa, jambo ambalo linatulazimu wakati mwingine kuwarudisha nyumbani mapema ili wakajisaidie huku muda wa kazi ukiwa bado ukiwa haujafika”
Licha ya mkoa huo kujitahidi kuboresha miundombinu ya shule zilizopomkoani humo na usimamizi makini, katika uandikishaji wa wanafunzi wa awali kwamwaka 2014 asilimia 79.4 ya wanafunzi waliandikishwa, na kwa upande wa darasala Saba ni asilimia 91 wakati mwenendo wa kuripoti shuleni kwa wanafunzi wakidato cha kwanza ni asilimia asilimia 84
Share
MATUKIO
Posted by Unknown
About the Author
Write admin description here..
«Newer Post
Older Post»
0 comments:
About Me
Unknown
View my complete profile
NiceMedia. Powered by
Blogger
.
BOFYA HAPA LIVE NICEMEDIA RADIO
Radio ya Injili inayoburudisha na Kuelimisha
Popular
Recent
Comments
Tags
Popular Posts
South Africa links Rwanda diplomats to attacks
Kenya anti-terrorism squad gets $735 a month
Waislamu waendelea kuuawa na Anti-Balaka CAR
kuzisha hati Milioni moja wakimbia machafuko Sudan Kusiniwa
PITIA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI DECEMBER 15, 2016
Labels
Afya
BURUDANI
Favourite
Gear
HABARI
HABARI ZA INJILI
HIVI PUNDE
MAGAZETI
MAKALA
MATUKIO
nice studio
SIASA
slider
TANGAZO
Nice Media work Tz
Latest tweets
Latest Videos From NiceMedia Prod.
Search
BLOG RAFIKI
Udaku Special
MillardAyo
Jiachie
Text Widget
© 2013
NiceMediaWorks
.
Woo Themes
converted by
Bloggertheme9
Blogger templates
. Proudly Powered by
Blogger
.
0 comments: