NiceMediaWorks
Home
Posts
Email
MATUKIO
HABARI
MAGAZETI
MAKALA
BURUDANI
AFYA
PRODUCTION
INJILI
Style Icons
MAWASILIANO
Top 10 List
Friday, May 30, 2014
WANANCHI WENYE HASIRA KALI WAMPIGA NA KISHA KUMCHOMA MOTO KIJANA MMOJA KWA TUHUMA ZA WIZI..Bofya hapa...
at 3:16:00 PM | 
No comments
Mwili wa Kijana huyo Ukiwa umefunikwa na Majani Kabla ya Kuchomwa Moto
Mwili wa Kijana huyo ukiwa unachomwa Moto na wananchi wa Eneo hilo
Akielezea Tukio Lilivyo tokea
Ng'ombe Walioibiwa
Wakichukua Mwili wa Kijana Huyo
Wakichukua Mwili wa Kijana Huyo
**********************
WAKATI vyombo mbali mbali zikiendelea na jitihada za kuwaelimisha wananchi juu ya madhara ya kujichukulia sheria mkononi hali hiyo bado ni tete mkoani Mbeya.
Hali hiyo imezidi kujitokeza baada ya Wananchi wenye hasira kali wa Mwasanga Ivumwe jijini Mbeya kumpiga na kumchoma moto mwananchi mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja wakimtuhumu kwa Wizi wa Ng’ombe mmoja na ndama.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ameuambia mtandao huu kuwa tukio hilo lilitokea mapema leo asubuhi ambapo chanzo ni wizi wa Ng’ombe wa Kongoro Mwakitalima mkazi wa Isyesye kata ya Ilomba.
Alisema Ng’ombe huyo aliibiwa jana majira ya usiku ambapo mzee huyo alitoa taarifa kwa majirani ambao asubuhi walijihimu kutafuta ambapo walipofika maeneo ya
Ivumwe walikutana na mwendesha boda boda ambaye aliwaambia amekutana na mtu akiwa anaswaga hiyo mifugo.
Alisema baada ya kusikia hivyo waliamua kuanza kumfukuzia wakitumia bodaboda na ndipo walipofika eneo la Mwasanga relini walimkuta mtuhumiwa akiwa na hao Ng’ombe.
Alisema Wananchi mbali mbali walikusanyika na kuanza kumshushia kipigo kutokana na eneo hilo kukithiri kwa wizi wa mifugo lakini baada ya kipigo hicho mtuhumiwa alionekana kuwa ngangari jambo lililowatia hasira na kuamua kumchoma moto.
Shuhuda huyo aliendelea kusema baada ya kuanza
kumchoma lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida mtu huyo hakuweza kukata roho hadi alipookolewa na Askari wa jeshi la polisi walipofika eneo la tukio.
Hadi tunaingia mtamboni hakuna taarifa zilizothibitisha kama mtuhumiwa huyo bado yuko hai ama amepoteza maisha.
Endelea Kufuatilia hapa hapa..
Share
MATUKIO
Posted by Unknown
About the Author
Write admin description here..
«Newer Post
Older Post»
0 comments:
About Me
Unknown
View my complete profile
NiceMedia. Powered by
Blogger
.
BOFYA HAPA LIVE NICEMEDIA RADIO
Radio ya Injili inayoburudisha na Kuelimisha
Popular
Recent
Comments
Tags
Popular Posts
South Africa links Rwanda diplomats to attacks
Kenya anti-terrorism squad gets $735 a month
Waislamu waendelea kuuawa na Anti-Balaka CAR
kuzisha hati Milioni moja wakimbia machafuko Sudan Kusiniwa
PITIA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI DECEMBER 15, 2016
Labels
Afya
BURUDANI
Favourite
Gear
HABARI
HABARI ZA INJILI
HIVI PUNDE
MAGAZETI
MAKALA
MATUKIO
nice studio
SIASA
slider
TANGAZO
Nice Media work Tz
Latest tweets
Latest Videos From NiceMedia Prod.
Search
BLOG RAFIKI
Udaku Special
MillardAyo
Jiachie
Text Widget
© 2013
NiceMediaWorks
.
Woo Themes
converted by
Bloggertheme9
Blogger templates
. Proudly Powered by
Blogger
.
0 comments: