NiceMediaWorks
Home
Posts
Email
MATUKIO
HABARI
MAGAZETI
MAKALA
BURUDANI
AFYA
PRODUCTION
INJILI
Style Icons
MAWASILIANO
Top 10 List
Tuesday, May 27, 2014
UPINZANI WAIBUA KASFA NYINGINE YA UFISADI BUNGENI..Chungulia hii...
at 3:59:00 AM | 
No comments
KAMBI rasmi ya upinzani bungeni imeibua ufisadi wa kutisha, kwamba Wizara ya Uchukuzi iliiagiza Mamlaka ya Bandari (TPA), ilipe gharama za sh milioni 11.164 katika Hoteli ya New Africa kwa ajili ya Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba.
Ufisadi huo uliibuliwa jana bungeni na Kambi Rasmi ya Upinzani kwenye hotuba yao kuchangia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2014/15.
Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Moses Machali (NCCR-Mageuzi), alisema malipo hayo kwa ajili ya malazi, yalifanyika Machi 28 mwaka jana.
“Mheshimiwa Spika, Machi 14 2013, Wizara ya Uchukuzi iliandika barua yenye kumb. Na. CB 230/364/01/A iliyoomba PTA ilipe gharama ya sh milioni 11.164 katika Hoteli ya New Africa kwa ajili ya Naibu Waziri wa Uchukuzi. Malipo haya yalilipwa na Bandari Machi 28, 2013. Malipo hayo hadi leo hayana maelezo.
Machali alisema ufisadi huo umeainishwa katika ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) kwa mwaka huu wa fedha.
Alisema katika taarifa ya CAG, haijaelezwa fedha hizo zililipwa kwa ajili ya shughuli gani zilizokuwa zikitekelezwa na Naibu Waziri huyo na shughuli hizo zilikuwa na maslahi gani kwa umma.
Kwa mujibu wa Machali, taarifa ya CAG ya mwaka 2012/2013 imebainisha kwamba kuna matumizi mabaya ya madaraka ndani ya Wizara ya Uchukuzi.
Alisema wizara hiyo imekuwa ikitoa miongozo mbalimbali kwa TPA ikiiagiza kufanya matumizi kwa ajili ya wizara hiyo kinyume na taratibu za utawala bora.
Katika mwaka wa fedha unaoishia Juni 30 mwaka 2013, Machali alisema CAG alibaini kuwa sh milioni 44.320 zililipwa na Bandari kwa niaba ya wizara hiyo.
Alisema kuwa Bandari ililipa sh milioni 18.156 kwa ajili ya kugharimia safari ya Naibu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Uchukuzi ya kwenda nchini Ghana kwa safari ya kikazi.
Alisema TPA ilipata mwaliko wa watu wanne kuhudhuria maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Afrika yaliyofanyika huko Accra, Ghana kuanzia Juni 16 hadi 23, 2013.
Aliongeza kuwa TPA ilimteua Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu kuiwakilisha Bandari na wizara ikamteua Naibu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu ili kuiwakilisha wizara katika maadhimisho hayo ambapo gharama za washiriki wote wawili ziligharamiwa na Bandari.
Share
MATUKIO
Posted by Unknown
About the Author
Write admin description here..
«Newer Post
Older Post»
0 comments:
About Me
Unknown
View my complete profile
NiceMedia. Powered by
Blogger
.
BOFYA HAPA LIVE NICEMEDIA RADIO
Radio ya Injili inayoburudisha na Kuelimisha
Popular
Recent
Comments
Tags
Popular Posts
South Africa links Rwanda diplomats to attacks
Kenya anti-terrorism squad gets $735 a month
Waislamu waendelea kuuawa na Anti-Balaka CAR
kuzisha hati Milioni moja wakimbia machafuko Sudan Kusiniwa
PITIA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI DECEMBER 15, 2016
Labels
Afya
BURUDANI
Favourite
Gear
HABARI
HABARI ZA INJILI
HIVI PUNDE
MAGAZETI
MAKALA
MATUKIO
nice studio
SIASA
slider
TANGAZO
Nice Media work Tz
Latest tweets
Latest Videos From NiceMedia Prod.
Search
BLOG RAFIKI
Udaku Special
MillardAyo
Jiachie
Text Widget
© 2013
NiceMediaWorks
.
Woo Themes
converted by
Bloggertheme9
Blogger templates
. Proudly Powered by
Blogger
.
0 comments: