Serikali ya Libya imeuomba Umoja wa Mataifa na jamii ya kimataifa iisaidie kupambana na ugaidi, huku ikifanya jitihada za kuzuia nchi hiyo isitumbukie katika ukosefu zaidi wa amani. Serikali ya Libya imesema kuwa, serikali ya mpito inataka isaidiwe kuung'oa ugaidi nchini humo na kwamba inataka vita dhidi ya ugaidi vianze haraka iwezekanavyo.
Ijapokuwa serikali ya Tripoli haijesema wazi inataka msaada wa aina gani, lakini nchi hiyo bado haina taasisi ya jeshi na polisi yenye nguvu.
Katika upande mwingine Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio linaloziwekea vikwazo meli zenye kusafirisha kinyume cha sheria mafuta kutoka katika maeneo ya Libya yanayodhibitiwa na makundi ya wanamgambo.
Azimio hilo, litaruhusu nchi wanachama wa Baraza la Usalama kukagua meli zinazodaiwa kubeba mafuta kinyume cha sheria kutoka Libya katika maji ya kimataifa.
Thursday, March 20, 2014
Libya yaomba msaada wa kukabiliana na ugaidi
at 2:05:00 AM |  No comments
Share
Posted by Unknown
0 comments: