Monday, June 13, 2016

Serikali yatumia Bilioni 2 kulipa Fidia ili kusaidia kukamilisha mradi wa ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami

at 6:24:00 AM  |  No comments

 Mhandisi wa Miradi (TANROADS) Mkoa wa Dar es salaam Bw.Ngusa Julius akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu ujenzi wa  Barabara zinazoendelea kujengwa ili  kupunguza msongamano  wa magari katika jiji La Dar es salaam, Kulia ni Afisa Habari wa wakala huo Bi Aisha Malima.
 Afisa Habari wa wakala wa Barabara (TANROADS) Bi Aisha Malima akitoa wito kwa wananchi kutunza barabara zinazojengwa na wakala huo ili ziweze kudumu kwa matumizi ya sasa na baadae.Kushoto ni  Mhandisi wa miradi Mkoa wa Dar es salaam Bw.Ngusa Julius.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa TANROADS na vyombo vya Habari leo jijini Dar es salaam uliolenga kutoa tathmini ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabra katika jiji la Dar es salaam inayolenga kupunguza tatizo la msongamano wa magari. Kulia ni Afisa Habari wa wakala huo Bi Aisha Malima.(Picha na frank Mvungi-Maelezo).


Frank Mvungi-Maelezo

Serikali yatumia Bilioni 2 kulipa Fidia ili kusaidia kukamilisha mradi wa ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami kati ya Tanki Bovu na Goba Jijini Dar es salaam.

Kauli hiyo imetolewa na Mhandisi wa Miradi wa TANROADS Mkoa wa Dar es salaam Bw. Ngusa Julius wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.Akifafanua Mhandisi Ngusa amesema kuwa fidia kwa wakazi hao itakamilika kulipwa wiki hii ili kazi ya ujenzi wa Barabara hiyo iweze kukamilishwa kwa wakati hali itakayosaidia kupunguza msongamano wa magari.

“Ujenzi wa barabara hii ukikamilika utasaidia kwa Kiasi kikubwa kupunguza foleni kwa kuwa itakuwa kiungo kati ya wakazi wa Mbezi Beach na Kimara na maeneo mengine ya jiji la Dar es salaam.” Alisisitiza Mhandisi Ngusa.Kwa upande wa Barabara ya kinyerezi Kifuru Mhandisi Ngusa amesema kuwa Milioni 431 zimetumika kulipa fidia na ujenzi wa Barabara hiyo unaendelea.

Miradi ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lamai inayotarajiwa kukamilika katika kipindi hiki cha mwaka wa fedha 2015/2016 itasaidia kupunguza msongamano wa magari kwa kiwango kikubwa katika jiji la Dar es salaam.Awamu ya Tatu ya ujenzi itahusisha barabara za Goba - Wazo hill -Tegeta Kibaoni (13.0Km), Mbezi Mwisho - Malambamawili- Kifuru (6kM), Goba - Makongo ardhi (9km ) na Pia kukamilisha usanifu wa outering road Bunju B - Mpiji Magohe - Victoria Kifuru hadi Pugu kiltex 33.7.

Wakala wa Barabara nchini TANROADS unatekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara katika jiji la Dar es salaam kwa kiwango cha lami ambapo barabara hizo zinatarajiwa kuondoa tatizo la msongamano wa magari katika jiji hilo.

Share
Posted by Unknown
About the Author

Write admin description here..

0 comments:

Text Widget

Blogger templates. Proudly Powered by Blogger.