Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dk. James
Mataragio (mbele) akielezea mikakati ya shirika hilo katika matumizi ya
gesi asilia inayozalishwa kwa ajili ya matumizi ya majumbani na
nyingine kuuzwa katika soko la nje katika kikao kilichokutanisha Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya
nishati, Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo kilichofanyika jijini Dar es
Salaam. Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kujadili matumizi ya gesi
iliyogunduliwa nchini katika matumizi ya ndani na nyingine kuuzwa nje
ya nchi.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya
nishati, Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo (pichani) akisisitiza jambo
katika kikao hicho.
Wataalam
kutoka Idara ya Nishati kutoka kushoto, Mussa Abbas na Athur Lyatuu
wakinukuu hoja mbalimbali zilizokuwa zinajadiliwa katika kikao hicho.
Wataalam
kutoka Idara ya Nishati iliyopo chini ya Wizara ya Nishati na Madini
wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa katika
kikao hicho.
0 comments: