NiceMediaWorks
Home
Posts
Email
MATUKIO
HABARI
MAGAZETI
MAKALA
BURUDANI
AFYA
PRODUCTION
INJILI
Style Icons
MAWASILIANO
Top 10 List
Tuesday, August 19, 2014
Umeipata hii?????PADRI WA JIMBO KATOLIKI LA MOSHI AONDOLEWA SAKRAMENT YA UPADRI NA PAPA FRANCIS NA KURUHUSIWA KUOWA
at 5:00:00 AM | 
No comments
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa
Francis
(PICHANI)amekubali kumuondolea sakramenti ya upadri,
Raymond
Mosha wa Jimbo Katoliki la Moshi
ikiwa
ni miaka 20 tangu padri huyo aombe kuachana na daraja hilo.
Barua ya uamuzi wa Papa Francis ilisomwa
juzi
katika parokia na vigango vyote vya Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi katika ibada zilizofanyika katika makanisa ya jimbo
hilo
.
Miongoni mwa parokia
ambazo
barua hiyo ilisomwa ni Karanga ambako Paroko wake, John Matumaini alitoa tangazo hilo katika ibada
zote
. Uamuzi huo ambao ni nadra kutolewa na Papa, unamaanisha kuwa sasa padri huyo yuko huru kuoa na kuwa na
familia
.
Hata hivyo, wakati uamuzi huo ukitangazwa rasmi juzi, tayari Padri Mosha ambaye ni profesa wa falsafa na maadili katika Chuo Kikuu cha
Nelson Mandela
Arusha
, ana mke na watoto watatu
ambao
kwa sasa wako vyuo vikuu.
Padri Mosha alisema aliandika barua kuomba kuondolewa daraja hilo mwaka
1994
kabla ya uamuzi kutolewa juzi.
Katika orodha ya mapadre 185 wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi iliyopo katika tovuti ya jimbo hilo, jina la
Padri
Mosha linaonekana likiwa ni namba 23.
Akizungumzia hatua hiyo, Padri Mosha alisema: “Ninafurahi kufunguliwa kifugo hiki na hii itanifanya niishi kama Mkristo. Kwa vile hawajaniondolea sifa ya kutoa huduma kama vile ibada za mazishi, sakramenti ya mwisho na ubatizo, nitaendelea kutoa kwa wahitaji kwa sababu ninaupenda ukristo.
“Nashukuru sasa nimekuwa
muumini
wa kawaida nitaweza kufunga ndoa kanisani kwa kuwa nilikuwa nimefunga ndoa ya kisheria tu kwa DC.”
Kuhusu kwa nini aliamua kuacha upadri, Profesa Mosha alisema ni baada ya kufanya kazi hiyo kwa miaka 20 na akaona ipo haja ya kuwa na familia lakini kanisa
lilikuwa
haliruhusu.
“Sasa kwa kuwa kanisa haliruhusu mapadri kuoa ndiyo maana nikaamua kuandika barua ambayo hata hivyo, imechukua muda mrefu kujibiwa na tayari nina watoto watatu wako chuo kikuu.
Share
MATUKIO
Posted by Unknown
About the Author
Write admin description here..
«Newer Post
Older Post»
0 comments:
About Me
Unknown
View my complete profile
NiceMedia. Powered by
Blogger
.
BOFYA HAPA LIVE NICEMEDIA RADIO
Radio ya Injili inayoburudisha na Kuelimisha
Popular
Recent
Comments
Tags
Popular Posts
South Africa links Rwanda diplomats to attacks
Kenya anti-terrorism squad gets $735 a month
Waislamu waendelea kuuawa na Anti-Balaka CAR
kuzisha hati Milioni moja wakimbia machafuko Sudan Kusiniwa
PITIA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI DECEMBER 15, 2016
Labels
Afya
BURUDANI
Favourite
Gear
HABARI
HABARI ZA INJILI
HIVI PUNDE
MAGAZETI
MAKALA
MATUKIO
nice studio
SIASA
slider
TANGAZO
Nice Media work Tz
Latest tweets
Latest Videos From NiceMedia Prod.
Search
BLOG RAFIKI
Udaku Special
MillardAyo
Jiachie
Text Widget
© 2013
NiceMediaWorks
.
Woo Themes
converted by
Bloggertheme9
Blogger templates
. Proudly Powered by
Blogger
.
0 comments: