NiceMediaWorks
Home
Posts
Email
MATUKIO
HABARI
MAGAZETI
MAKALA
BURUDANI
AFYA
PRODUCTION
INJILI
Style Icons
MAWASILIANO
Top 10 List
Thursday, August 14, 2014
HII NI HATARI...MPIGA DEBE AUAWA KWA KUPIGWA KISU KISA DENI LA SH.2000 TU..Chungulia hapa ujionee...
at 2:10:00 AM | 
No comments
Mwili wa mpiga debe huyo baada
ya
kifo chake
DENI la Sh 2,000 limetosha kumaliza uhai wa mpiga debe maarufu wa stendi ya mabasi yaendeayo mikoani ya mjini Iringa, Samwel Yengayenga baada ya kuchomwa kisu
mara
mbili katika eneo la mgongoni na kifuani.
Tukio hilo la kinyama limetokea jana majira ya saa 6:.55 mchana baada ya Yengayenga na mtuhumiwa wa mauaji yake aliyekuwa akidai kiasi hicho cha fedha kurushiana maneno makali na kisha kupigana.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Festo Ruben Mkalala (26), muosha magari, mkazi wa mjini Iringa ambaye alikamatwa mara baada ya kufanya tukio hilo.
Mungi alisema Yengayenga, Mkalala na mtu mwingine wa
tatu
(hakumtaja jina) wanadaiwa siku nne zilizopita waliosha basi la Kimotco linalofanya
safari
zake kati ya Iringa na Arusha.
“Stahiki ya kazi hiyo ilikuwa Sh 15,000; hata hivyo hawakulipwa fedha hizo baada ya kumaliza kazi hiyo,” alisema.
Alisema siku iliyofuata Mkalala na kijana huyo mwingine waliyefanya naye kazi walikwenda kuchukua ujira wao na kugawana Sh 5,000 kila mmoja huku Mkalala akiahidi kutunza Sh 5,000 za Yengayenga mpaka watakapokutana.
Walipokuta, RPC alisema Mkalala alimpa Yengayenga Sh 3,000 badala ya Sh 5,000 na kuahidi kummalizia kiasi kilichobaki kesho yake.
Kitendo hicho kwa mujibu wa mashuhuda kinadaiwa kumchukiza Yengayenga aliyeamua kunyanganya simu ya Mkalala mpaka amaliziwe Sh2,000 zake zilizobaki.
Kamanda Mungi alisema Mkalala alichukizwa na uamuzi huo na kuanzisha ugomvi uliopeleka kifo cha Yengayenga.
“Uchunguzi wa awali unaonesha Mkalala aliamua kupigana na Yengayenga ili arudishiwe simu yake na alipozidiwa alikimbia kusikojulikana na kurudi akiwa na kisu mkononi,” alisema.
Ili kuipata simu yake, Kamanda Mungi alisema ushahidi wa awali unaonesha Mkalala alitumia kisu hicho kumchoma mgongoni na kifuani Yengayenga na kusababisha mauti yake.
Yengayenga alikufa papo hapo katika tukio ambalo mtuhumiwa huyo alikamatwa na kufikishwa kituo cha Polisi cha kati cha mjini Iringa.
Share
MATUKIO
Posted by Unknown
About the Author
Write admin description here..
«Newer Post
Older Post»
0 comments:
About Me
Unknown
View my complete profile
NiceMedia. Powered by
Blogger
.
BOFYA HAPA LIVE NICEMEDIA RADIO
Radio ya Injili inayoburudisha na Kuelimisha
Popular
Recent
Comments
Tags
Popular Posts
South Africa links Rwanda diplomats to attacks
Kenya anti-terrorism squad gets $735 a month
Waislamu waendelea kuuawa na Anti-Balaka CAR
kuzisha hati Milioni moja wakimbia machafuko Sudan Kusiniwa
PITIA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI DECEMBER 15, 2016
Labels
Afya
BURUDANI
Favourite
Gear
HABARI
HABARI ZA INJILI
HIVI PUNDE
MAGAZETI
MAKALA
MATUKIO
nice studio
SIASA
slider
TANGAZO
Nice Media work Tz
Latest tweets
Latest Videos From NiceMedia Prod.
Search
BLOG RAFIKI
Udaku Special
MillardAyo
Jiachie
Text Widget
© 2013
NiceMediaWorks
.
Woo Themes
converted by
Bloggertheme9
Blogger templates
. Proudly Powered by
Blogger
.
0 comments: