NiceMediaWorks
Home
Posts
Email
MATUKIO
HABARI
MAGAZETI
MAKALA
BURUDANI
AFYA
PRODUCTION
INJILI
Style Icons
MAWASILIANO
Top 10 List
Wednesday, May 7, 2014
MKUU WA MAJESHI AKWEPA KUZUNGUMZIA KAULI ZA WANASIASA JUU YA JESHI KUPINDUA NCHI
at 4:51:00 AM | 
No comments
Arusha,Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange,juzi amekwepa kuzungumzia au kutoa ufafanuzi kuhusu kauli zinazotolewana baadhi ya viongozi wa kisiasa kuwa iwapo muundo wa serikali tatu utapitishwa,Jeshi la Wananchi wa Tanzania wa Tanzania (JWTZ) linaweza kupindua nchini.Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano mkuuwa nane wa Wakuu wa Idara za Ukaguzi za Majeshi (DIWG) kutoka nchi zaJumuiya ya Maendeleo za Kusini mwa Afrika (SADC), Jenerali Mwanyange,alisema hawezi kujiingiza katika masuala ya siasa.Alitoa jibu hilo kufuatia swali aliloulizwa na mwandishi kuhusu anakauli kauli gani kufuatia baadhi ya viongozi kulihusisha jeshihilo na siasa .“Siwezi kujibu hilo swali, siwezi kujiingiza katika haya masuala. ni sawa mimi mchezaji wa mpira wa miguu uniulize swali kuhusu mpira watennis” alisema na kusisitiza aulizwe kuhusiana na mkutano unaoendelea.
Baadhi ya wanasiasa, wamekuwa wakitoa kauli, katika bunge maalum la Katiba kuwa, kama muundo wa Serikali tatu, ukipita wataingia msituni na wengine wakisema jeshi linaweza kupindua nchi kwani serikali ya Muungano inayopendekezwa katika rasimu ya Katiba, itakuwa na jukumu la kulipa mishahara ya majeshi lakini haina mapato ya uhakika.Mapema akifungua mkutano huo jijini hapa jana, Jenerali Mwamunyange,aliwataka wakuu wa idara za ukaguzi katika majeshi ya SADC,kuhakikisha majeshi yao yanakuwa tayari wakati wowote kutekelezamajukumu yao.Alisema ukaguzi wa majeshi ni jambo muhimu ili kujua iwapo yapo tayarikutekeleza majukumu yao katika kulinda amani, usalama wa mipaka yanchi wanawachama. Akizungumzia mkutano huo, Mwenyekiti wa(DIWG) BornwellNjilika alisema chombo hicho cha wakaguzi wa majeshi kinakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwepo upungufu wa fedha na uchache wa watumishi wa makao makuu waliopo Botswana.Katika mkutano huo, Tanzania iliteuliwa kuwa mwenyekiti mpya wa DIWG chini yaBrigedia Jenerali Emmanuel Edward Maganga.
Share
MATUKIO
Posted by Unknown
About the Author
Write admin description here..
«Newer Post
Older Post»
0 comments:
About Me
Unknown
View my complete profile
NiceMedia. Powered by
Blogger
.
BOFYA HAPA LIVE NICEMEDIA RADIO
Radio ya Injili inayoburudisha na Kuelimisha
Popular
Recent
Comments
Tags
Popular Posts
South Africa links Rwanda diplomats to attacks
Kenya anti-terrorism squad gets $735 a month
Waislamu waendelea kuuawa na Anti-Balaka CAR
kuzisha hati Milioni moja wakimbia machafuko Sudan Kusiniwa
PITIA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI DECEMBER 15, 2016
Labels
Afya
BURUDANI
Favourite
Gear
HABARI
HABARI ZA INJILI
HIVI PUNDE
MAGAZETI
MAKALA
MATUKIO
nice studio
SIASA
slider
TANGAZO
Nice Media work Tz
Latest tweets
Latest Videos From NiceMedia Prod.
Search
BLOG RAFIKI
Udaku Special
MillardAyo
Jiachie
Text Widget
© 2013
NiceMediaWorks
.
Woo Themes
converted by
Bloggertheme9
Blogger templates
. Proudly Powered by
Blogger
.
0 comments: