Meneja
wa NMB Kanda Lecrisia Makiriye (Kulia) Akikabidhi Msaada wa Mashuka
kwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Dk. Mary Mwanjelwa ambaye pia ni M-NEC Taifa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)
BENKI ya Nmb Kanda ya Nyanda za
Juu Kusini imekabidhi msaada wa Madawati na mashuka vyenye thamani ya Shilingi
Milion 10 kwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya(CCM) Dk. Mary Mwanjelwa.
Msaada huo ni pamoja na
madawati 83 na mashuka 250 ambavyo Mbunge huyo alikabidhiwa na Meneja wa Kanda
wa NMB katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Benki hiyo zilizopo Mbalizi
Road jijini Mbeya.
Akizungumza wakati wa
makabidhiano hayo, Meneja wa NMB Kanda, Lecrisia Makiriye, alisema benki ya NMB
inatoa huduma zake katika jamii ya watu mbali mbali kwa kuwa ndiyo wadau
wanaofanya Benki hiyo kupata maendeleo.
Alisema katika msaada wa leo
Benki hiyo imetoa mashuka 250 kwa ajili ya Hospitalini na Madawati 83 kwa ajili
ya wanafunzi wa Shule za Msingi ndani ya Mkoa wa Mbeya ambao shule zao
zinaupungufu wa madawati.
Alisema sehemu ya mashuka hayo
Mashuka 100 atapeleka kwa waliokumbwa na mafuriko hivi karibuni wilayani Kyela
na mashuka mengine 150 atapeleka kwa wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa wa
Mbeya.
Alisema Madawati atayagawa
katika Shule za Msingi zenye upungufu ndani ya Mkoa wa Mbeya kadri
itakavyowezekana kutokana na mahitaji ya madawati kuwa bado makubwa katika
kuinua kiwango cha Elimu mkoani Mbeya.
Aidha alitoa wito kwa taasisina watu binafsi kuendelea kujitolea kwa msaada wa hali na mali kwa wananchi waWilaya ya Kyela kutokana na mafuriko yaliyowakuta kwamba bado hali zaohazijatengemaa hivyo jitihada zaidi zinahitajika.
0 comments: