NiceMediaWorks
Home
Posts
Email
MATUKIO
HABARI
MAGAZETI
MAKALA
BURUDANI
AFYA
PRODUCTION
INJILI
Style Icons
MAWASILIANO
Top 10 List
Monday, May 5, 2014
BUNGE LA BAJETI LAWEKEWA UTARATIBU MPYA WA KUCHAGIA HOJA DAKIKA ZAPUNGUZWA KUTOKA 15 MPAKA 7
at 3:01:00 AM | 
No comments
Wabunge wa Bunge la Bajeti linaloanza kesho mjini Dodoma, wamepunguziwa muda zaidi wa kuchangia kutoka dakika 15 hadi saba.
Bunge hilo la Bajeti limetengewa siku chache ambazo zitalilazimu kuendeshwa kwa kasi ili kukamilisha shughuli zake.
Habari zilizopatikana jana zilisema hatua hiyo inatokana na muda kuwa mfupi kwa kuwa Bunge hilo litakutana kwa siku 52 ikiwa ni pungufu ya siku 28 ikilinganishwa na mkutano kama huo wa mwaka jana.
Katibu wa Bunge, Thomas Kashililah alipoulizwa kuhusu taarifa hiyo jana alisema ofisa habari wa Bunge, Owen Mwandumbya angeweza kulizungumzia. Hata hivyo, Mwandumbya alipoulizwa alisema atazungumza leo.
Miongoni mwa marekebisho yaliyopitishwa katika kupunguza muda wa vikao ni pamoja na kuendelea kufanyika hadi Jumamosi pia kumalizika saa 2:00 usiku.
Ratiba iliyotolewa na Bunge imesema utaratibu wa sasa unalilazimisha lifanye uamuzi wake (kupitisha au kutokupitisha), Bajeti ya Serikali pamoja na Sheria za Fedha ifikapo mwishoni mwa Juni kila mwaka, ili kuruhusu utekelezaji wa bajeti husika kuanza Julai Mosi, siku ya kwanza ya mwaka mpya wa fedha.Chanzo:Mwananchi
Share
MATUKIO
Posted by Unknown
About the Author
Write admin description here..
«Newer Post
Older Post»
0 comments:
About Me
Unknown
View my complete profile
NiceMedia. Powered by
Blogger
.
BOFYA HAPA LIVE NICEMEDIA RADIO
Radio ya Injili inayoburudisha na Kuelimisha
Popular
Recent
Comments
Tags
Popular Posts
South Africa links Rwanda diplomats to attacks
Kenya anti-terrorism squad gets $735 a month
Waislamu waendelea kuuawa na Anti-Balaka CAR
kuzisha hati Milioni moja wakimbia machafuko Sudan Kusiniwa
PITIA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI DECEMBER 15, 2016
Labels
Afya
BURUDANI
Favourite
Gear
HABARI
HABARI ZA INJILI
HIVI PUNDE
MAGAZETI
MAKALA
MATUKIO
nice studio
SIASA
slider
TANGAZO
Nice Media work Tz
Latest tweets
Latest Videos From NiceMedia Prod.
Search
BLOG RAFIKI
Udaku Special
MillardAyo
Jiachie
Text Widget
© 2013
NiceMediaWorks
.
Woo Themes
converted by
Bloggertheme9
Blogger templates
. Proudly Powered by
Blogger
.
0 comments: