NiceMediaWorks
Home
Posts
Email
MATUKIO
HABARI
MAGAZETI
MAKALA
BURUDANI
AFYA
PRODUCTION
INJILI
Style Icons
MAWASILIANO
Top 10 List
Thursday, April 24, 2014
WARIOBA AFUNGUKA KWA KUWAULIZA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM MASWALI 7 YA MSINGI..Pitia hiiiiii...
at 4:07:00 AM | 
No comments
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba ameuliza maswali saba ya msingi kwa wajumbe wa Bunge la Katiba wanaopinga Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume yake akitaka wawajibu wananchi ili kutuliza kiu yao.
Jaji Warioba ambaye tangu awasilishe Rasimu ya Katiba Desemba 30, mwaka jana amegeuka kuwa adui kwa watu wanaotaka muundo wa serikali mbili, aliuliza maswali hayo jana katika uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa Taasisi ya Twaweza kuhusu mchakato wa Katiba.
Akizungumza kwa ukali, Jaji Warioba alisema: "Kwanza, jibuni kwa nini mnapinga muundo wa Muungano wakati walioupendekeza ni wananchi?
"Sheria inasema uwepo wa Muungano na mapendekezo katika rasimu hayasemi Muungano usiwepo. Kumbukeni kuwa wananchi walitakiwa kutoa mapendekezo ya namna ya kuboresha Muungano."
Katika swali lake la pili, Warioba alisema kwa nini Tanganyika imevaa koti la Muungano? Kwa kuwa katika ukusanyaji wa maoni wananchi walieleza kuwa Serikali ya Muungano ya sasa siyo ya Muungano, ni ya Tanganyika.
Katika swali la tatu alisema wajumbe hao wanatakiwa kujibu maelezo ya wananchi ambao waliieleza tume hiyo kuwa Katiba imevunjwa na madaraka ya rais yamechukuliwa na sasa kuna marais wawili katika nchi moja.
"Tume inapewa lawama kubwa, wajibuni wananchi hii tume ilitumwa na nani kukusanya maoni ya wananchi? Waambieni ilikusanya maoni hayo kwa kutumia sheria ipi zaidi ya ile ya Mabadiliko ya Katiba?" alisema Jaji Warioba katika swali lake la nne.
Katika swali lake la tano, Warioba aliwataka wajumbe hao kutoa sababu za kumtuhumu kuwa amependekeza muundo wa serikali tatu kwa sababu yeye pamoja na (Joseph Butiku) walikuwa wajumbe wa Tume ya Jaji Kisanga na Jaji Nyalali ambazo nazo zilipendekeza muundo wa serikali tatu, kitu ambacho alisema si kweli na hawakuwahi kuwa mjumbe wa tume hizo.
Pia, aliwataka wajumbe hao kujibu swali la sita, kwa nini hawataki kuzungumzia yaliyomo katika Rasimu ya Katiba na badala yake wanageuza rasimu hiyo kuwa imeandikwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Katika swali lake la saba, aliwataka wajumbe kujibu kwa nini wanaishutumu Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuwa imeingiza maoni yake, wakati ilikusanya maoni hayo kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba?
Alisema badala ya kujadili hoja za msingi, wajumbe wa Bunge hilo wamekuwa wakitoa lugha za kejeli na matusi kwa baadhi ya watu (akiwamo na yeye), kitendo ambacho alisema si sahihi na kinaweza kuligawa taifa kwa sababu yaliyomo katika Rasimu ya Katiba yametokana na maoni ya wananchi.
Katika uzinduzi huo walikuwepo baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo ambao ni Dk Hamisi Kigwangalla aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Julius Mtatiro, Maria Sarungi na aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole.
Share
MATUKIO
Posted by Unknown
About the Author
Write admin description here..
«Newer Post
Older Post»
0 comments:
About Me
Unknown
View my complete profile
NiceMedia. Powered by
Blogger
.
BOFYA HAPA LIVE NICEMEDIA RADIO
Radio ya Injili inayoburudisha na Kuelimisha
Popular
Recent
Comments
Tags
Popular Posts
South Africa links Rwanda diplomats to attacks
Kenya anti-terrorism squad gets $735 a month
Waislamu waendelea kuuawa na Anti-Balaka CAR
kuzisha hati Milioni moja wakimbia machafuko Sudan Kusiniwa
PITIA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI DECEMBER 15, 2016
Labels
Afya
BURUDANI
Favourite
Gear
HABARI
HABARI ZA INJILI
HIVI PUNDE
MAGAZETI
MAKALA
MATUKIO
nice studio
SIASA
slider
TANGAZO
Nice Media work Tz
Latest tweets
Latest Videos From NiceMedia Prod.
Search
BLOG RAFIKI
Udaku Special
MillardAyo
Jiachie
Text Widget
© 2013
NiceMediaWorks
.
Woo Themes
converted by
Bloggertheme9
Blogger templates
. Proudly Powered by
Blogger
.
0 comments: