NiceMediaWorks
Home
Posts
Email
MATUKIO
HABARI
MAGAZETI
MAKALA
BURUDANI
AFYA
PRODUCTION
INJILI
Style Icons
MAWASILIANO
Top 10 List
Friday, April 18, 2014
RAIS KIKWETE ATUNUKIWA TUZO YA UTUMISHI BORA NA HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA....Ingia hapa...
at 12:23:00 PM | 
No comments
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akipokea Tuzo ya Utumishi Bora wa Umma Barani Afrika kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe (kulia) kufuatia mchango mkubwa alioutoa kwa maendeleo ya wananchi wa Tanzania na Bara la Afrika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akisoma ujumbe ulioandikwa kwenye Tuzo ya Utumishi Bora wa Umma Barani Afrika aliyokabidhiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe (kulia) leo Ikulu jijini Dar es salaam
.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe (kulia) akisoma ujumbe ulioandikwa kwenye cheti kilichoambatana na Tuzo ya Utumishi Bora wa Umma Barani Afrika aliyokabidhiwa Rais Jakaya Kikwete leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe (kulia) akimkabidhi
Rais Jakaya Kikwete (kushoto) cheti kilichoambatana na Tuzo ya Utumishi Bora wa Umma Barani Afrika
leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo Ikulu jijini Dar es salaam amepokea Tuzo ya Utumishi Bora wa Umma Barani Afrika kufuatia mchango mkubwa alioutoa kwa maendeleo ya wananchi wa Tanzania na Bara la Afrika.
Akiwa mwenye furaha mara baada ya kupokea tuzo hiyo ambayo awali ilipokelewa kwa niaba yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe jijini Washngton Marekani, Rais Kikwete amesema kuwa ameipokea tuzo hiyo kwa moyo wa shukrani na heshima kubwa kufuatia imani kubwa iliyoonyeshwa kwake na kwa watanzania.
“Nimeipokea tuzo hii kwa moyo wa ukunjufu, ni tuzo ya watanzania wote kwa sababu mambo yote niliyoyafanya sikuwa peke yangu nimeyafanya kwa kushirikiana na watanzania wote” Amesema Rais Kikwete.
Rais Kikwete amesema kuwa amepokea tuzo hiyo kufuatia wasomaji na wadau wa Jarida la African Leadership Magazine ambalo huchapishwa mjini London, Uingereza na mjini Washington kuonyesha imani juu yake kwa kumchagua kwa njia ya kura ya maoni kama kiongozi aliyetoa mchango mkubwa zaidi kwa maendeleo ya wananchi wake katika Bara la Afrika kwa mwaka 2013.
“Nawashukuru sana African Leadership Magazine, kwangu ni heshima kubwa nawaomba watanzania tuendelee kushirikiana wenzetu duniani wanaona, wanatambua na kuthamini mchango wetu” Amesisitiza Rais Kikwete.
Awali kabla ya kumkabidhi Rais Jakaya Kikwete Tuzo hiyo na cheti cha shukrani Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe amesema kuwa tuzo hiyo ni heshima kwa taifa la Tanzania kufuatia juhudi kubwa alizoonyesha Rais Jakaya Kikwete katika kuboresha maisha ya watanzanzania.
Amesema kuwa wasomaji na wadau wa jarida maarufu la kimataifa la African Leadership Magazine wamemuona Rais Kikwete kuwa Kiongozi Bora wa Afrika aliyetoa mchango mkubwa zaidi katika maendeleo ya kiuchumi ya wananchi wake kwa mwaka 2013 kwa kumpigia kura nyingi za maoni.
Aidha ameeleza kuwa Rais Kikwete alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo katika sherehe kubwa iliyotangazwa na kuonyeshwa moja kwa moja na mitandao mbali mbali ya kijamii duniani pia kuhudhuriwa na watu mbali mbali mashuhuri wakiwemo mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Marekani na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mheshimiwa Job Ndugay ambaye alikuwa Washington kikazi.
Wengine ni Mwakilishi katika Bunge la Wawakilishi wa Jimbo la Georgia nchini Marekani na mwenyekiti wa wabunge weusi katika Bunge hilo, Bi. Dee Dawkins-Haigler na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mheshimiwa Liberata Mulamula.
Rais Kikwete amepata tuzo hiyo akimfuatia Rais wa Sierra Leone , Mheshimiwa
Ernest Bai Koroma, ambaye alishinda Tuzo hiyo mwaka 2012.
Share
MATUKIO
Posted by Unknown
About the Author
Write admin description here..
«Newer Post
Older Post»
0 comments:
About Me
Unknown
View my complete profile
NiceMedia. Powered by
Blogger
.
BOFYA HAPA LIVE NICEMEDIA RADIO
Radio ya Injili inayoburudisha na Kuelimisha
Popular
Recent
Comments
Tags
Popular Posts
South Africa links Rwanda diplomats to attacks
Kenya anti-terrorism squad gets $735 a month
Waislamu waendelea kuuawa na Anti-Balaka CAR
kuzisha hati Milioni moja wakimbia machafuko Sudan Kusiniwa
PITIA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI DECEMBER 15, 2016
Labels
Afya
BURUDANI
Favourite
Gear
HABARI
HABARI ZA INJILI
HIVI PUNDE
MAGAZETI
MAKALA
MATUKIO
nice studio
SIASA
slider
TANGAZO
Nice Media work Tz
Latest tweets
Latest Videos From NiceMedia Prod.
Search
BLOG RAFIKI
Udaku Special
MillardAyo
Jiachie
Text Widget
© 2013
NiceMediaWorks
.
Woo Themes
converted by
Bloggertheme9
Blogger templates
. Proudly Powered by
Blogger
.
0 comments: