NiceMediaWorks
Home
Posts
Email
MATUKIO
HABARI
MAGAZETI
MAKALA
BURUDANI
AFYA
PRODUCTION
INJILI
Style Icons
MAWASILIANO
Top 10 List
Tuesday, April 22, 2014
NINI UHALALI WA CCM KUKATAA RASIMU YA WARIOBA???WASOMI WAHOJI... Pitia hapa ujionee..
at 5:37:00 AM | 
No comments
Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Jaji Frederick Werema
Baadhi ya wasomi na wanahakati wamehoji ni wapi Chama Cha Mapinduzi (CCM wanapata uhalali wa kuikataa rasimu ya katiba na kuitaka itoe ushahidi kuwa mapendekezo yaliyomokwenye rasimu iliyoandaliwa na Tume ya Warioba si maoni ya wananchi.
Wakizungumza na NIPASHE katika mahojiano, walisema haitoshi kusema maoni si halali bila kutoa ushahidi. Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambao majina yanahifahiwa kuepusha kulumbana na chama na serikali walisema hata kama ni mkakati wa chama kithibitishe madai hayo.
“Wajumbe wa CCM wanaojiita kundi la wengi wanaikataa rasimu kuwa yaliyomo si maoni ya wananchi, tungependa ieleze inapata wapi uhalali wa kuyakataa?
“ Wananchi walitakiwa waihoji ili ilete ushahidi siyo kuendeeleza malumbano kwa kutumia takwimu ambazo kila mjumbe anazitafsiri anavyotaka,” alisema mhadhiri mtaalamu wa taaluma za uongozi.
Alisema mchakato wa katiba ya Tanzania haikufanyika kama Afrika Kusini ambayo katiba iliandikwa na Bunge Maalumu la Katiba kama lilivyo la Dodoma lenye wanasiasa na wajumbe wanaowakilisha makundi mbalimbali ya kijamii.
Alisema wajumbe hao baada ya bunge kuundwa kisheria walijigawanya kwenye kamati mbalimbali kama ilivyofanyika kwa bunge la Tanzania na kuunda tume ndogo miongoni mwao iliyowaendea wananchi kukusanya maoni.
“Wajumbe walikusanya maoni kwenye mikutano, mtandao, simu, barua na mabaraza, baada ya kazi walirudi bungeni na ripoti ambayo bunge zima liliitumia kuandika katiba ya Afika Kusini huru,” aliongeza mmojawapo.
Walifafanua kuwa wajumbe walioko Dodoma hawakukusanya maoni isipokuwa Al-Shaymaa Kwegyir , ndiye mbunge pekee aliyekuwa kwenye Tume ya Warioba, hivyo hawana uhalali wa kuikataa rasimu.
“Kama wangekuwa kwenye Tume ya Warioba wangeweza kuthibitisha kuwa maoni si ya wananchi kwani wana ushahidi hawakuwepo hawana uthibitisho, wasivuruge mchakato,” alionya mhadhiri mwingine wa siasa.
Alisema kwa sababu mchakato haukuwa kama wa Afrika Kusini wajumbe wasiendeleze madai aliyoyaita ya uongo kuikataa rasimu.
Kwa upande wake Mwanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, anayefuatilia mchakato huo, Harold Sungusia, alisema CCM inaposema maoni si ya wananchi inaakisi msimamo iliowahi kuutoa zamani.
Alisema Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema, na aliyekuwa Waziri wa Sheria, Celina Kombani, walisema Tanzania haihitaji katiba mpya.
Alionya kuwa huenda chama tawala kinaendelea na fikra kuwa katiba iliyopo inahitaji kuwekewa viraka na kuendelea kutumika ndiyo sababu ya kuibua madai kama hayo.
Sungusia alisema labda wajumbe hao waeleza kuwa maoni na matakwa ya CCM hayakuzingatiwa kwenye rasimu hiyo, lakini si kudai yaliyomo siyo maoni ya wananchi.
Alikumbusha kuwa CCM hakikuwa na mpango wa kuandika katiba mpya na ilani yake haikuwahi kutaja suala hilo na kwamba mchakato huo umetokana na uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete na siyo wa CCM.
ALiongeza kuwa tangu mwanzo CCM ilikataa suala la Muungano lisijadiliwe kwenye mchakato wa kuandika katiba mpya na sasa inaibuka kwa sura nyingine .
Alisema kwa sababu kilichosumbua ni Muungano ushauri ulitolewa kuwa hoja irudi kwa wananchi kupitia kura ya maoni Watanzania waseme wanataka uwe wa namna gani lakini CCM ilikataa pia mapendekezo hayo.
Alisema kama CCM inakataa maoni ikubali sasa kuitisha kura ya maoni ya taifa zima kujadili suala la Muungano na muundo wa serikali badala ya kuleta muundo wa serikali inayoupenda.
Rasimu ya katiba imependekeza serikali tatu jambo linalipingwa na CCM na kusababisha malumbano baina yake na wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao sasa wamesusia bunge hilo ambalo leo litaendelea na vikao.
CHANZO: NIPASHE
Share
MATUKIO
Posted by Unknown
About the Author
Write admin description here..
«Newer Post
Older Post»
0 comments:
About Me
Unknown
View my complete profile
NiceMedia. Powered by
Blogger
.
BOFYA HAPA LIVE NICEMEDIA RADIO
Radio ya Injili inayoburudisha na Kuelimisha
Popular
Recent
Comments
Tags
Popular Posts
South Africa links Rwanda diplomats to attacks
Kenya anti-terrorism squad gets $735 a month
Waislamu waendelea kuuawa na Anti-Balaka CAR
kuzisha hati Milioni moja wakimbia machafuko Sudan Kusiniwa
PITIA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI DECEMBER 15, 2016
Labels
Afya
BURUDANI
Favourite
Gear
HABARI
HABARI ZA INJILI
HIVI PUNDE
MAGAZETI
MAKALA
MATUKIO
nice studio
SIASA
slider
TANGAZO
Nice Media work Tz
Latest tweets
Latest Videos From NiceMedia Prod.
Search
BLOG RAFIKI
Udaku Special
MillardAyo
Jiachie
Text Widget
© 2013
NiceMediaWorks
.
Woo Themes
converted by
Bloggertheme9
Blogger templates
. Proudly Powered by
Blogger
.
0 comments: